Pages

January 9, 2012

WEMA AMWANGUKIA BABA YAKE

Na Musa Mateja
BAADA ya kuandamwa na skendo kibao ‘bandika bandua’, hatimaye Wema Isaac Sepetu, anadaiwa kufunga safari hadi visiwani Zanzibar kwenda kumwangukia baba yake mzazi, Isaac Abraham Sepetu, Ijumaa Wikienda lina fulu data.
MGUU KWA MGUU NA MAMA YAKE
Habari za uhakika zilisema kuwa Wema aliondoka Dar es Salaam tangu Januari 4, mwaka huu akiambatana na mama yake mzazi, Mariam Sepetu ambaye kwa sasa ni ‘mashosti’ baada ya kukataa kurudi kwa ‘bwa’mdogo’ Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Ilielezwa kuwa mbali na mambo mengine, Wema alikwenda kumuomba msamaha baba yake kwa matukio yake yote ambayo yamekuwa yakimtokea ikiwemo suala la kuvishwa pete ya uchumba na msanii Diamond bila kumshirikisha.
IJUMAA WIKIENDA LAIVU NA WEMA
Baada ya kutia kibindoni mpango mzima, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lilizungumza na Wema ambaye alikiri yupo nyumbani kwa baba yake, Zanzibar.


BABA YAKE ANAUMWA
Staa huyo aliyefunika kwenye muvi ya Dj Ben inayosumbua kitaani, alisema aliamua kwenda kumjulia hali mzazi wake kwa sababu anaumwa (hakutaka kuelezea kinachomsumbua baba yake).
Wema aliweka kweupe kuwa alikuwa na muda mrefu hajaonana na baba yake hivyo alihitaji kuzungumza naye.

AMEKWENDA KUMWANGUKIA?

Kuhusu kumwangukia baba yake kufuatia mambo mengi ambayo yamepita hapo nyuma, Wema alisema ni kweli kupitia nafasi hiyo amepata muda wa kubadilishana mawazo na kupata ushauri zaidi wa kimaisha kutoka kwa baba na mama yake wakiwa visiwani humo.
Alifunguka: “Nimeinjoi kukaa na baba kwani naona maisha yanaenda freshi, nimepata baraka kutoka kwa wazazi wangu wote wawili, jambo ambalo nililimisi kwa muda mrefu.

WEMA MPYA?

“Natarajia kurudi Dar baada ya siku mbili hivi nikiwa mpya kabisa, nimefarijika sana.”

BADO HALI SI SHWARI

Hivi karibuni Wema aliingia kwenye gogoro zito na mpenzi wake Diamond baada ya kumtuhumu kucheza ‘nje kapu’ kimapenzi na Jokate Mwegelo ambapo hadi sasa hali si shwari.
No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...